02
May

Nduru Za Mwananchi by Grammo Suspect-Rainbow Ambassador Kenya (single)

#NduruZaMwanaNchi

Verse 1

Wuuuuuuuuuuuui,Jehovah Gai,kila mahali nduru

Watu wamepoteza uhai,sisi Mungu katunusuru

Wame kimbilia Dubai,wengine wame fanywa viguru

Mahoya ma Pastor Lai,dahoya makinye iguru

Ati nihame wanadai,juu naitwa Mburu

Juu wao warabai,wanadhani wata niamuru

Jamani hii haifai,Kenya ni huru

Yaumiza why lie,Mwananchi napiga nduru

Luo au Masai,nipe haki ya kuzuru

Jiji kubwa Nai,nikipenda pia Nakuru

Niuze machungwa mapapai Lamu pia Limuru

Niuzie Chebet au Kantai,nikikosa nisi fukuru

Kwenye basi na safiria,ghafla naskia nduru

Barabarani watu wana angalia,kando yao magurudumu

Hewani(sniffing) damu yanukia,msalaba mwekundu wahudumu

Basini bomu kalipukia,alshabaab kachukua jukumu

Ugaidi umezidi kupindukia,Vifo wanahukumu

Maisha wana katsia,hakuna atakae dumu

Ni wapi wana ingililia,au tunao wahujumu?

Serikali tuna waangalia,hili ni lenu jukumu

Wakristo Waislamu pia,tuchunge ulimi sumu

Moto sote waturukia,kuuzima ni ngumu

Kuwa Mkenya siwezi jutia,milele nitaishi humu

Mapenzi nitazingatia,jirani, mwah mwah nita mchumu

Chorus

Kila mahali Nduru

Giza hakuna nuru

Mwananchi napiga nduru

Nadai kuwa huru

Verse 2

Hawa wanasiasa laghai,chanzo cha nduru

Uongo yenu madai,ati mwataka kutunusuru

Kikombe cha chai,ana kuitia Raisi Uhuru

Ni dharau unadai,kiburi una jiskia guru

Maneno mengi kutuhadai,uchochezi nchi unadhuru

Mwa sababisha vurumai,mwaturudisha enzi za makuburu

Utadhani mwavuta ngwai,zenu kakara kukuru

Mna udhi walai,mwatubeba kama kunguru

Wakati wa Moi,bado mlitudhuru

Wakati wa Mwai,mkazidi tupigisha nduru

Sasa referendum mwadai,utumike wetu ushuru?

Wapi Yash Pal Ghai,si tulipanga misururu?

Baba while you are here,Mpeketoni wanapiga nduru

Huja fanya cha kusaidia,vitendawili ujuha kalulu

Tana river of tears, wana tamani wahamie Buruburu

Habari za Wajir,ana tupasha binti Hassan Lulu

Kenya mzima tunalia, giza hakuna nuru

Kamwe hatuta wakubalia,kutubeba kikalulu

Juu mnavyo nitania,mwafurahia zangu nduru

Ni kama mwaswalia,serikali isi faulu

Kiti mpate kukalia,mpate ongeza ndururu

Hamna cha kuhofia,zogo ikizuka Bombolulu

Watoto wenu hawatalia,wanatalii Honolulu

Chorus

Kila mahali Nduru

Giza hakuna nuru

Mwananchi napiga nduru

Nadai kuwa huru

Verse 3

Serikali ,kufunga tai,siko kuli wapeleka ikulu

Kutalii hadi Hawai,mkitumia wetu ushuru

Mna drive kubwa ndai,mie tao mguu toka Kamulu

Wengine suruali hatuvai,ukosefu wa ndururu

Asubuhi sinywi chai,mchana kutwa nimeshika sururu

Natamani viazi karai,minyoo inapiga nduru

Wewe unaraukia divai,mara sima na zumburu

Serikali miili ina rai,Mwananchi mnyonge nazulu

Damu ilimwagika mkoloni aki fukuzwa Kenya tukapata uhuru

Wakenya waka panga misururu,waka chagua raisi anaitwa Uhuru

Iweje mimi mkimbizi ndani yaNchi yangu sina uhuru?

We Raisi Uhuru,hii ni ukoloni mambo leo hatutaki ,tunataka u-hu-ru

Mkenya nani nilisai,risasi zalia kama guruguru?

Naogopea wangu uhai,natamani ishi kama chururu

Maongezi Raila anakurai,unakuwa mkali kama muru

Ni dharau unadai,kiburi ita kumaliza Uhuru

Uhuru na kazi ulidai,ufisadi umeshindwa sulu

Deepak khamani Laghai,ndie tunalipa ushuru

Mwezi mzima sasa Mpeketoni bado wanapiga nduru

Nchi mzima kuki haribika,kweli utaweza kutu nusuru?

Mauti kama matlai kila mahali nduru

Namshukuru Wangari mathai,alale salama huyu guru

Wengine mwajifanya masheikh na hamfai,jioni mwajifanya kufuturu

Hamna uchungu ni kama hamzai,Olelenku,Kimaiyo,Ruto na uhuru

Mkishindwa kulinda Nchi,naomba mjiuzulu

Kwani mie Mwananchi,nime choka kupiga NDURU

Chorus

Kila mahali nduru

Giza hakuna nuru

Mwananchi napiga nduru

Nadai kuwa huru