02
May

Mama by Grammo Suspect ft Nas Chavez-Rainbow Ambassador Kenya (single)

#MAMA

Intro- This song goes to my mama, and everybody else who is a mama

Verse 1

Nilipo kuwa mdogo uli nibeba kwa mgongo

Mama uka nitunza, na pia uka ni funza

Na nilipo potoka, huku sema wewe toka

Mbali uli ni komesha na uka zidi ni somesha

Na tazama miaka ya nyuma ulipo kuwa uki nilea

Njaa kote Nchini ilikuwa ime enea

Lakini uli ng’ang’ana na kubanana na shida zote,za mitaa yaani balaa

Mimi kiumbe Grammo,uli nilea bila chapaa

Na uka nifunza Mama kuto kata tamaa

Machozi mara kwa mara mimi huni bubujika

Niki kumbuka kazi ngumu ulio jitwika,nipate elimika

Mara zingine mama, wewe uli ugua

Lakini mama wee , uka endelea piga dua

Mara zingine mama,mimi nili ku kosea

Lakini mama wee uka endelea niombea…

Chorus

Nakupenda sana,mamangu mpenzi

Nina kutukuza,kwa hayo yako malezi

Ume nitunza,toka hizo enzi

Kwa kweli mama,unafaa hizi pongezi

Verse 2

Sijui niseme nini ili upate niamini

Kwani watu flani wana sema mi muhuni

Lakini toa shaka mama hayo mawazo duni

Hao ni wambea na naomba,uzidi kuwaombea

Wengine wakwambia kwamba Ma’ nakula dawa

Nami nasema kwamba Ma’, wao wame pagawa

Mimi natambua kwamba Yesu ndie ndawa

Ali nipa kipawa,napepea bila mabawa

Na mama hapo nyumbani wewe unapo nikosa

Mahali nilipo mimi si ati nafanya makosa

Mbali napiga dili,ili umasikini nipate ku ukabili

Au labda maisha nipate kuya badili

Kwani bonge la Safari na safiri

Yataka utulivu uangalifu,haitaki ukatili

Mienendo mbaya mimi sina budi kubadili

Chorus

Nakupenda sana,mamangu mpenzi

Nina kutukuza,kwa hayo yako malezi

Ume nitunza,toka hizo enzi

Kwa kweli mama,unafaa hizi pongezi

Verse 3

Nachukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mola

Aliye nipa Mama huyu mwenye roho poa

Sina haya nikisema mamangu hana madola

Lakini pendo lake bora kuliko madola

Kwa hivyo Mungu na kuomba uzidi kumbariki

Nakupa uhakika kuwa sita kusaliti

Na pia umtunze ,na mimi uniguze

Nipate toka kwani Grammo ,sijui nitoke vipi

Tazama ni wakati wangu kumtunza,

Lakini ni mtunze vipi kama mi’ sija sijewi lo!

Lakini no,siwezi kata tamaa na sauti naipaza

Nikitangaza kuwa mimi nisha anza kujikaza,niki pakaza

Naomba tafadhali mama,omba na mimi kisha uimbe na mimi

Omba na mimi kisha uimbe na mimi…

Chorus

Nakupenda sana,mamangu mpenzi

Nina kutukuza,kwa hayo yako malezi

Ume nitunza,toka hizo enzi

Kwa kweli mama,unafaa hizi pongezi

Outro- Grammo the Suspect,Nas Chavez