02
May

Hypocrisy by Grammo Suspect-Rainbow Ambassador Kenya (EMBRACE DIVERSITY)

#Hypocrisy

Intro

Ukifungua pazia,uone zao ghasia

Nkt nkt nkt

Now this is Grammo Suspect- Rainbow Ambassador Kenya

Ukipenda,niite Mtetezi wa Raiaa

Au sio,hahaa

Chorus

Hii ni ya wenye homophobia

Njoo niku treat na four beers

Nikupe mistari kama mia

Bila shaka uta nivulia kofia

Hii ni ya wenye HOMOPHOBIA

Rekebisheni zenu mbaya tabia

Wacheni,kujifanya ngamia

Tuishi real yaani mia kwa mia

Verse 1

Una jifanya righteous,chini ya maji we poko.

Hollier than thou,mwili yako ni soko

Stealing in the name of the Lord,wewe ni umbwa koko.

Preaching hate,wacha udoko.

Wewe muislamu,mkononi una mboko

Ume sahau ni haramu,bado una leta unoko.

Mali ya uchawi,usione usonko.

Chai si lazima majani,waweza tumia cocoa.

Chuki huleta zogo please,tumia ubongo.

Kenya ndio home,siwezi hamia Bongo.

So let me be,siwezi ishi uwongo

Na mi, mtu mzima,siwezi cheza kalongo

Siwezi cheza kalongo

Na mi mtu mzima siwezi cheza kalongoo

Chorus

Hii ni ya wenye homophobia

Njoo niku treat na four beers

Nikupe mistari kama mia

Bila shaka uta nivulia kofia

Hii ni ya wenye HOMOPHOBIA

Rekebisheni zenu mbaya tabia

Wacheni,kujifanya ngamia

Tuishi real yaani mia kwa mia

Verse 2

Wengi nawajua walio fuga majini

Na mbio huenda mosque,wakiskia mwadhini.

Wangapi huji fanya,watu wa dini,

Na usiku mchana,kazi yao kuzini?

Wengi wame vaa, official,juu chini

Kumbe ndani ya suti wame ficha upini

Swali ni jee,ngozi ya kondoo,tuta vua lini?

Hakuna aliye clean,hapa duniani.

Living as I am,sio kuwa muhuni

Kaumbwa nilivyo, si mambo ya kubuni

Kwa mfano wake,alie Binguni.

Chorus

Hii ni ya wenye homophobia

Njoo niku treat na four beers

Nikupe mistari kama mia

Bila shaka uta nivulia kofia

Hii ni ya wenye HOMOPHOBIA

Rekebisheni zenu mbaya tabia

Wacheni,kujifanya ngamia

Tuishi real yaani mia kwa mia

Verse 3

Yooo

Hii ni ya wale wame bonga sana, usha kuta?

Uki hisi pupuu, follow the loo,usi ite choo njoo

Hapa niko fresh,no smell ya mkojo

Tena chapchap,si mwendo wa jongoo

Nafanya mambo yangu,sifuati kikondoo

Strong and tough,si bebwi kwa mgongoo

Hapa kwangu hutosh,hata ulete usongo

Am living my life,zangu ndoto

Niko conscious,siko ngoto

Nina choma sana,over maji Moto

Panga ya kata kuwili, kulia,kushoto

Basi bebi njoo,nikupe uhondo

Na kama wataka more,basi hapo chonjo

Chorus

Chonjo,chonjo,kila kitu chonjoo

Chonjo,chonjo,kila kitu,chonjooo × 2

Outro

Yaah Man

LGBT,

LOVE IS LOVE

EMBRACE DIVERSITY